Rais samia ametujengea shule ya vipaji maalumu kumuenzi bibi titi

"Wakati tunazindua awamu ya kwanza ya tamasha la Bibi Titi tulipata baraka ya kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa Rais wa kwanza mwanamke na wakati huo ilikuwa ni miezi michache tangu aapishwe kuwa Rais mwaka 2021.

Rais Samia alitupa wosia wake kutuelezea mambo aliyofanya Bibi Titi na anavyoona sisi tunavyopaswa kufanya vijana wa karne hii, yale ambayo yalifanywa na Bibi Titi na yale ambayo anatamani kuona vijana wa leo tunayafanya kuenzi mchango mkubwa ambao Bibi Titi aliujenga kwa taifa letu.

Kwa mwaka huu tunategemea Mh.Rais ndiye ataadhimisha, kama ni yeye mwenyewe au kwa namna atakavyoona inafaa kuadhimisha siku ya kufunga maadhimisho haya ambayo itakuwa ni tarehe 3 mwezi disemba.

Kuanzia tarehe 27 yapo matukio mengi yatakayofanyika, na lazima tumpongeze Mh Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kujenga shule ya wasichana wenye vipaji maalum Rufiji yenye thamani ya takribani bilioni nne mpaka sita ambayo inatambulika kama Bibi Titi Mohamed Secondary school."- Mohamed Mchengerwa,Waziri wa TAMISEMI

Share: