Ziwa albert: watu 20 wamekufa kwa kuzama majini na zaidi ya tani tano za bidhaa zilizoagizwa uganda

Takribani watu 20 wamekufa maji jimboni Ituri na zaidi ya tani tano za bidhaa zilizoagizwa Uganda zimezama Jumatano, Mei 15, katika Ziwa Albert kufuatia kuzama kwa boti, Radio Okapi ya nchini Drc imeripoti.

Kulingana na Huduma ya Ulinzi wa Raia huko Ituri, tukio hili linatokana na upepo mkali uliovuma Aprili iliyopita kwenye Ziwa Albert.

Serikali imehusisha janga hili la asili na mabadiliko ya tabia nchi.

Mratibu wa huduma hiyo, Robert Ndjalonga alidokeza kuwa hali hii inaathiri shughuli za usafiri wa ziwani na uvuvi ambazo ni hatari sana.

Ili kuzuia upotevu wa maisha ya binadamu na uharibifu wa nyenzo, imeshauriwa kwa wavuvi, wasafirishaji na wateja kujipanga na jaketi za kuokoa maisha kila wakati na kupunguza shughuli kwenye Ziwa Albert.

Share: