
Wanaume wanne wamekamatwa baada ya picha za Donald Trump na mkosaji Jeffrey Epstein aliyepatikana na hatia kuonyeshwa kwenye kasri la Windsor siku ya Jumanne, wakati rais huyo wa Marekani akiwasili nchini Uingereza kwa ziara ya kiserikali.
Walikamatwa kwa tuhuma za "mawasiliano mabaya kufuatia kukwama kwa umma huko Windsor" na kusalia kizuizini, Polisi wa Thames Valley walisema.
Waliokamatwa ni wanaume watatu mmoja mwenye umri wa miaka 60 kutoka East Sussex, mwenye umri wa miaka 36 na mwenye umri wa miaka 50 kutoka London, na mwenye umri wa miaka 37 kutoka Kent.
Kikosi hicho kilisema uchunguzi unaendelea baada ya maafisa kudhibiti "haraka" picha hizo na kusitisha kuonekana kwa picha hizo kwenye kasri hiyo, ambapo Trump amekutana na Mfalme Charles katika siku ya kwanza kamili ya ziara yake ya kitaifa.
Urafiki wa Trump na Epstein umeanza miaka mingi sana. Kuna picha za tangu miaka ya 90 zikionyesha wawili hawa kuwa pamoja wakati Epstein alipohudhuria harusi ya Trump.
Mwaka 2002, Trump alimuelezea Epstein kama "mtu mzuri sana", baadae Epstein akasema alikuwa rafiki wa karibu wa Trump kwa takribani miaka kumi.
Urafiki wao uliyumba miaka ya 2000, kama miaka miwili tu kabla Epstein hajakamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na shutuma hizo za ngono.
Wakati ikulu ya Whitehouse ilisema Trump alivunja urafiki na Epstein kwasababu ya tabia zake za ajabu ajabu – gazeti la Washington post linasema walipishana kwenye maswala ya biashara ya majengo huko Florida.