WATU 15 WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUBADIKA SSH 2530 BILA KIBALI

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu 15 waliokuwa wanatumia namba za gari za SSH 2530 baada ya Septemba Mosi mwaka huu Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime kutoa onyo ya matumizi ya namba hizo.

Misime alitangaza baadhi ya watu kubandika namba hizo kwenye magari yao kinyume na sheria ambapo ilikuwa inaanza kuchukua sura mpya ya kuendelea kubandikwa kwa namba hizo.

Mtu yeyote anayebandika namba hizo baada ya kufuatiliwa kwenye mifumo ya usajili, itahesabika hilo ni kosa la kisheria na atakayekamatwa atakuwa anatuhumiwa kwa kosa la kuendesha chombo cha moto bila ya kuwa na usajili wa namba rasmi.

Hayo yamesemwa leo Septemba 4, 2025 na Kamanda wa Kanda hiyo Jumanne Muliro alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 Marejeo ya Mwaka 1973 yaliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, mtu yeyote anayeendesha chombo cha moto bila kuwa na usajili rasmi na namba halali za usajili anatenda kosa la jinai.

"Ni makosa na swala hili ni kosa kisheria kwa sababu namba hizi hazipo kwenye mfumo wa usajili wa vyombo vya moto lakini pia ni kinyume cha sheria za usalama barabarani," amesema Kamanda Muliro.

Share: