Watu wawili wameuawa katika jumla ya mashambulizi 20 ambayo Zelensky amesema yamezilenga nyumba, barabara na hospitali eneo hilo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi ya Urusi katika eneo la mashariki la Kherson na kuyaita "mashambulizi ya kigaidi."
Watu wawili wameuawa katika jumla ya mashambulizi 20 ambayo Zelensky amesema yamezilenga nyumba, barabara na hospitali eneo hilo.
Kulingana na utawala wa kijeshi wa Ukraine, mkoa wa Kherson ulioko katika mto Dnipro umekuwa ukilengwa kwa mashambulizi ya Urusi na kuanzia Jumamosi pekee, karibu mabomu 400 yamefyetuliwa eneo hilo. Mapigano yameripotiwa katika maeneo mengine kama Mariinka, Avdiivka na Bakhmut.
Ukraine imekuwa ikikabiliana na uvamizi wa Urusi uliodumu kwa zaidi ya miezi 21, na mashambulizi yake ya kujihami yaliyozinduliwa katika majira ya joto mwaka huu, hadi sasa bado hayajakidhi matarajio yake.