WIZARA YA AFYA YATOA TAARIFA MUHIMU KUHUSU ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA UVIKO 19

Imekufikia na nimuhimu kuzingatia haya...

Taarifa kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Tanzania , imetoa tahadhari kwa wananchi wake kuhusu magonjwa yaenezwayo na mbu na magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa.


Katika taarifa hiyo rasmi Wizara imeeleza kuwa tangu Februari hadi Aprili 2025, ufuatiliaji umeonesha ongezeko la visa vya UVIKO-19 kutoka asilimia 1.4 (wagonjwa 2 kati ya watu 139 waliopimwa) mwezi Februari hadi asilimia 16.3 (wagonjwa 31 kati ya 190 waliopimwa) mwezi Machi, na kisha asilimia 16.8 (wagonjwa 31 kati ya watu 185 waliopimwa) mwezi Aprili 2025. Hali ya kuongezeka na kupungua kwa ugonjwa huu imekuwepo kila mwaka tangu kutangazwa kwa ugonjwa huu mwaka 2020. Kwa kipindi hiki ongezeko hili linaonekana zaidi katika mkoa wa Dar es Salaam.

Share: