Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dr. Damas Daniel Ndumbaro akishirikiana na wizara ya mambo ya nnje na ushirikiano wa africa mashariki pamoja na taasisi zake na ubalozi wa Cuba wamekuja na tamasha la kimataifa la kiswahili
Kungamano hili ni kwaajili ya kubidhaisha lugha ya kiswahili kutokana na mkakati uliozinduliwa na muheshimiwa makamu wa raisi Dr philip isdori mpango mnamo tarehe 7 julai 2022 na nia kuu ilikuwa ni kuitangaza lugha ya kiswahili nnje ya nnchi.
Kutokana na hotuba ya wizara ya utamaduni sanaa na michezo iliyosomwa bungeni mwaka huu ilielezwa kufunguliwa kwa vituo mia moja vya kufundishia kiswahili nnje ya nnchi na vitaendeshwa na watanzania wenye mafunzo kutoka baraza la kiswahili BAKITA na baraza la kiswahili Zanzibar bado lengo kubwa likiwa ni lile lile kuibidhaisha kiswahili nnje za nnchi kwahiyo pia italeta ajira kwetu sote kwasababu lugha ya kiswahili ni utamaduni wetu Tanzania. Licha ya hayo yote pia sanaa ya Tanzania inaendelea kuwa maarufu duniani kwasababu ya matumizi ya lugha yetu ya kiswahili hiyo ndio maana halisi ya kubidhaisha kiswahili.
Tamasha hili kubwa litafanyika Cuba na mgeni rasmi atakuwa mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan akiambatana na mwenyeji wake rais wa Cuba pia mawaziri wa nnchi zote mbili watakuwepo na washiriki zaidi ya 600 kwenye Tamasha hili wakitokea nnchi mbali mbali
Kwanini Cuba? "Tulikuwa tunajua tumepiga hatua kubwa kuitangaza kiswahili lakini sivyo kwani wataalamu na wachambuzi wamepinga hilo na ndio maana tumeamua kuja na Tamasha hili kutokana na kiswahili kwa lugha yako na tumechagua Havvana kutokana na tunataka kiswahili kwa kiispanyola ndiomana tukaichagua Cuba na mwaka mwingine tutaongeza lugha zingine." Amesema Dr Ndumbaro.
Matukio muhimu katika tamasha hilo ni:-
Hotuba ya uzinduzi ambayo itashereheshwa na marais wawili wa Tanzania na rais wa Cuba,
pia kutakua na masimulizi ya mahusiano ya watu wa Cuba na ya watu wa Tanzania ni kivipi tutaweza kuchangamana nao.
pia tutakuwa onesho la khanga maana hii ndio asili yetu wa Tanzania na ndiomana khanga huandikwa kwa maneno ya kiswahili.