Waziri dkt. doroth gwajima imekifungia kituo cha 'massage' cha tia massage & spa

Serikali kupitia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima imekifungia kituo cha huduma za 'Massage' cha TIA Massage & SPA cha Nzasa-Kijitonyama baada ya Video ya Tangazo lake kuripotiwa kuwa na Vitendo vilivyo kinyume na maadili. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara, huduma zimesitishwa kuanzia Oktoba 26, 2023 kutokana na kutokidhi vigezo vya Sheria Namba 23 ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, pia mmiliki ametozwa faini ya Tsh. Laki 5 pamoja na maelekezo mengine ambayo kama atayakiuka atafikishwa Mahakamani. 

Aidha, Wizara imetoa mawasiliano ya moja kwa moja ili kuripoti masuala mbalimbali kwa 0734 986503 na 026 2160250, matukio ya Ukatili wa Watoto namba 116 Saa 24. Na iwapo Waziri mwenye dhamana atahitajika, tuma ujumbe kwa namba 0765 345777 na 0734 124191.

Share: