Waziri bashungwa awataka wamiliki wa majengo kuwatumia wataalamu walio sajiliwa na bodi za crb, erb na aqrb

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa amezielekeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) na Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) kufika mara moja eneo la Magogoni kulipotokea tukio la kuanguka kwa jengo la ghorofa mbili na kushirikiana na timu za Wataalam kutoka Mamlaka nyingine za Serikali kupata sababu ya kuanguka jengo hilo na kuchukua hatua stahiki kwa wale wote ambao wamekiuka Sheria za kitaaluma katika ujenzi na usimamizi wa jengo hilo.

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ya leo Aprili 18, 2024 imebainisha kuwa Bashungwa amezitaka Bodi hizo kuhakikisha wanaendelea kusimamia miradi ya ujenzi ikiwemo barabara, madaraja na majengo na kuhakikisha wajenzi na wasimamizi wa miradi hiyo wanafanya kazi kwa kuzingatia miko na maadili ya taaluma zao.

Waziri Bashungwa anatoa pole kwa majeruhi na familia iliyopoteza mpendwa wao na anatoa wito kwa Wakandarasi, Wahandisi na wamiliki wa majengo kuhakikisha wanatumia wataalam waliosajiliwa na Bodi za CRB, ERB na AQRB ili kuepusha kutokea kwa madhara yanayoweza kusababisha majeruhi na vifo, na hivyo kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Share: