Watu wawili wameuawa na wengine saba kujeruhiwa katika "shambulio la makusudi" dhidi ya msafara wa misaada katika mji mkuu wa Sudan Khartoum, Shirika la Msalaba Mwekundu limesema.
Magari hayo - ambayo shirika misaada ya kiutu lilisema "yalikuwa na alama ya Msalaba Mwekundu" - yalitakiwa kuwahamisha zaidi ya raia mia moja.
Wafanyakazi wawili wa ICRC wameuawa katika shambulizi hilo na wengine saba wamejeruhiwa.
ICRC inasema jeshi na wanamgambo wa RSF walikuwa wamewahikishia usalama wafanyakazi wake wanaposafirisha mamia ya raia kuelekea maeneo salama lakini walishambuliwa.
Hayo yanajiri baada ya viongozi wa kikanda kusema viongozi wa jeshi la Sudan na wa kikosi maalum cha wanamgambo cha RSF wamekubaliana kufanya mazungumzo ya amani na kusitisha vita ambavyo vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kuwaacha watu milioni sita bila ya makazi Sudan.