Watu wanne wa familia tajiri zaidi nchini uingereza wamehukumiwa kifungo cha gerezani kwa kuwadhulumu wafanyakazi wao

Watu wanne wa familia Tajiri zaidi nchini Uingereza wamehukumiwa kifungo cha gerezani kwa tuhuma za kuwadhulumu wafanyakazi wao waliotoka India kuwahudumia katika makazi yao ya Geneva Villa.

Prakash na Kamal Hinduja, pamoja na mwana wao wa kiuma Ajay na mkewe Namatra wamepatikana na hatia ya kuwadhulumu wafanyakazi wasio kuwa na stakabadhi rasmi za kuishi au kufanya kazi.

Mahakama ya nchini Uswizi iliwahukumu vifungo vya kati ya miaka minne hadi minne na nusu

Wanne hao walipatikana hawana makosa kwa shtaka la ulanguzi wa watu, shtaka ambalo lina adhabu kali.

Mawakili wanaowawakilisha washtakiwa wamesema kwamba watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Akizungumza nje ya mahakama, wakili Robert Assael alisema, ‘nimeshtushwa sana, na tutakata rufaa na kupigana hadi mwisho.’

Wafanyakazi watatu waliosafirishwa kutoka India , wamesema kwamba familia hiyo iliwalipa pauni EURO 7 au dola 8 za Kimarekani kufanya kazi kwa saa kumi na nane , kiwango ambacho ni kidogo sana kuliko kinachokubalika chini ya sheria ya Uswizi.

Aidha walidai kwamba familia hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na mali ya thamani ya EURO bilioni 375 – ilikuwa haiwapi fursa ya kutoka nje ya makazi yao iliyopo katika mtaa ghali zaidi mjini Geneva.

Share: