Watu wa nne wamepoteza maisha katika ajali ya lori na coaster

Watu wanane wamefariki dunia na wengine wanane wamejeruhiwa baada ya coaster kugongana na lori asubuhi leo December 24, 2024 katika Kitongoji cha Kwachuma, Kata ya Segera, Tarafa ya Mkumburu, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga kwenye Barabara Kuu ya Segera-Chalinze.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili T.7800RL, aina ya Sharkman, likiwa na tela namba T.692 EJH likiendeshwa na Dereva Yohana Stephano, (35), Mkazi wa Goba Dar es salaam likitokea Tanga kuelekea Dar es Salaam na gari lenye namba za usajili T.906 DPJ, aina ya Toyota Coaster, mali ya Naman Joel Mkumbo, likiendeshwa na Thomas Hunay Gidahonda. (33) Mkazi wa Dar es salaam likitokea Dar es Salaam kuelekea Kilimanjaro”

“Ajali ilitokea baada ya Dereva wa Toyota Coaster kushindwa kulimudu gari lake na kupeleke kuyumba na kuelekea upande wa pili wa barabara, hali iliyosababisha kugongana uso kwa uso na gari hiyo aina ya Lori na kupelekea vifo vya Wanaume watano na Wanawake watatu”

“Majeruhi katika ajali hiyo ni Godlisen Hamphrey Minja (20), Mfanyabiashara, Mkazi wa Mabibo Dar es salaam, Riziki Severin Mboya, Dereva (28) Mkazi wa Njapanda Moshi, Lina Victus Swai (25), Mfanyabiashara, Gospan Wingod Lema (24) Fundi Umeme na Mkazi wa Temeke Dar es Salaam, Loyce Nuhu James (27) Mkazi wa Buguruni Dar es Salaam, Lucy Mathew Urio (24), Mkazi wa Dar es salaam na majeruhi wawili wa lori ambao ni Dereva wa lori Yona Stephano Madandi (35) Mkazi wa Goba Dar es salaam na Utingo wake Samweli Adinani Hossen. (24),Mkazi wa Dar es salaam”

Share: