Watu kumi wamefariki dunia baada ya helikopta mbili za jeshi la wanamaji kugongana angani

Watu kumi wamefariki dunia baada ya helikopta mbili za jeshi la wanamaji kugongana angani wakati wa mazoezi ya kijeshi ya gwaride la Wanamaji wa Kifalme Malaysia.

Moja ya ndege hizo ilinasa parapela ya ndege nyingine kabla ya zote kuanguka chini, kulingana na video iliyoonyeshwa na vyombo vya habari vya ndani.

Tukio hilo lilitokea saa 09:30 kwa saa za huko katika mji wa Malaysia wa Lumut, ambao ni kitovu cha kambi ya jeshi la wanamaji.



Hakuna manusura walioonekana.

"Waathiriwa wote walithibitishwa kuwa wamefariki kwenye eneo la tukio huku mabaki yakipelekwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lumut kwa utambulisho," Jeshi la Wanamaji la Kifalme la Malaysia lilisema, Imeongeza kuwa itaunda kamati kuchunguza chanzo cha tukio hilo.

Moja ya helikopta, HOM M503-3 ikiwa na watu saba, inaaminika kuanguka kwenye njia ya ndege.

Nyingine, Fennec M502-6 iliyokuwa imebeba waathiriwa wengine watatu, ilianguka kwenye kidimbwi cha kuogelea kilichokuwa karibu.

Idara ya zimamoto na uokoaji ya jimbo hilo ilisema iliarifiwa kuhusu tukio hilo saa 09:50 kwa saa za ndani (01:50 GMT).









Share: