Polisi walisema wahusika walilipwa ili kumuua AKA
Washukiwa 6 wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya rapa maarufu wa Afrika Kusini, Kiernan Forbes, maarufu kama AKA, na rafiki yake wa karibu, mpishi maarufu na mjasiriamali Tebello "Tibz" Motshoane.
Wawili hao waliuawa kwa kupigwa risasi nje ya mkagawa mmoja mjini Durban mwaka mmoja uliopita, katika mauaji ambayo yaliwashangaza mashabiki wengi wa muziki.
Polisi walisema wahusika walilipwa ili kumuua AKA lakini hakuna sababu ilifichuliwa ya lengo hilo Washukiwa hao, wote wenye umri wa chini ya miaka 36, wanatazamiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi.
"Ilikuwa wazi kwamba AKA alifuatiliwa kutoka uwanja wa ndege na Tibz hakuwa mlengwa aliyekusudiwa katika mauaji kwenye Barabara ya Florida huko Durban," Luteni Jenerali Nhlanhla