Watu 15 wamepoteza maisha wakati kimbunga na dhoruba zilipokumba maeneo ya marekani

Takribani watu 15 wamepoteza maisha wakati kimbunga na dhoruba zilipokumba maeneo ya kati ya Marekani, na kuharibu nyumba na kukata umeme kwenye makazi ya mamia kwa maelfu ya watu.

Watu saba walipoteza maisha kaskazini mwa Texas, watano huko Arkansas, wawili huko Oklahoma na mmoja huko Kentucky.

Wengine wengi walijeruhiwa, na karibu wakazi 500,000 hawakuwa na umeme katika majimbo kadhaa siku ya Jumapili.

Gavana wa Texas Greg Abbott alisema zaidi ya theluthi moja ya kaunti zote katika jimbo lake sasa zinakabiliwa na tangazo la maafa.

Sheriff Ray Sappington wa Kaunti ya Cook, Texas, alisema idadi ya waliofariki hapo ni pamoja na watoto wawili wenye umri wa miaka miwili na mitano na watu watatu wa familia moja.

"Ni uchafu sasa uliosalia," alisema sheriff wa eneo la Valley View, ambalo lilikuwa miongoni mwa yale yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga kikali.

Radi, ngurumo na mvua kubwa wakati huo huo zililazimisha kuhamishwa kwa watu wapatao 125,000 huku mbio za Jumapili za Indianapolis 500 zikiahirishwa kwa saa nne.

Share: