Mamlaka za Serikali zimetoa angalizo kuwa mitetemeko zaidi inaweza kutokea
Tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa 6.2 Richa limesababisha vifo vya Watu 105 katika Jimbo la Gansu, vifo 11 katika Jimbo la Qinghai na kujeruhi wengine 250.
Imeeleza kuwa Nyumba 4,782 zimeathirika na zoezi la uokoaji linaendelea.
Mamlaka za Serikali zimetoa angalizo kuwa mitetemeko zaidi inaweza kutokea, baada ya mitetemeko mingine 10 kurekodiwa katika maeneo ya Tibetani.
Share: