Wanne mbaroni kwa wizi wa choo cha bilioni 15

choo hicho cha dhahabu kinachoitwa "Amerika," kiliwekwa kwenye Jumba la Blenheim, kama sehemu ya maonyesho

London, watu wanne wameshtakiwa baada ya choo cha dhahabu chenye thamani ya karibu dola milioni 6 (zaidi ya Sh. bilioni 15) kuibiwa kutoka Blenheim Palace, alikozaliwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Winston Churchill.

Wizi huo ulifanyika Septemba 2019 wakati choo hicho cha dhahabu kinachoitwa "Amerika," kilipowekwa kwenye Jumba la Blenheim, kama sehemu ya maonyesho ambapo watu walialikwa kutumia choo hicho, takribani maili 65 kaskazini magharibi mwa London.

Choo hicho kilikuwa kimewekwa kwa siku mbili pekee kabla ya wizi huo kutokea na Polisi wa Thames Valley walipokea ripoti ya wizi huo katika jumba hilo saa 4:57 asubuhi Septemba 14, 2019, wakisema kuwa wahalifu hao walivamia usiku kucha na kuondoka eneo la tukio. saa 4:50 asubuhi.

Share: