Waliotukana familia ya rais Museven wafikishwa mahakamani

Waliotukana Familia ya Rais Museven wafikishwa mahakamani

David Ssengozi anayejulikana pia kwa jina la Lucky Choice (21) na Isaya Ssekagiri (28) walifikishwa mbele ya Hakimu Stella Maris Amabilis ambaye ameamuru waendelee kukaa chini ya ulinzi katika gereza la Kigo kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi iliyofunguliwa dhidi yao ya kuitusi familia ya Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo kwenye mtandao wa TikTok.

Wawili hao pamoja na mshtakiwa wa tatu Julius Tayebwa (19), wanakabiliwa na mashtaka ya kutoa matamshi ya chuki na kueneza taarifa ovu dhidi ya familia ya Rais.

Share: