Walinzi watano binafsi wamekamatwa kwa kujaribu kumpiga risasi waziri wa madini uganda

Walinzi watano Binafsi wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kumpiga risasi Waziri wa Maendeleo na Madini, Phiona Nyamutoro nchini Uganda.

Waziri huyo alikuwa ameambatana na Kaimu Kamishna wa Madini, Agnes Alaba kukagua Migodi ya Madini ya chuma yaliyopo Butare, Wilayani Rubanda, mali ya National Cement Company Limited ambayo ni Kampuni tanzu ya Devki Group.

 

Hapo jana Viongozi walitumia muda katika kikao cha mashauriano na wachimbaji Madini kutoka mkoa wa Kigezi katika eneo la White Horse Inn Kabale Wilayani Kabale kujadili usajili wa wachimbaji Madini unaoendelea kwa njia ya kibayometriki nchini kote. 

Hata hivyo, walipofika katika maeneo ya uchimbaji Madini leo Alhamisi, viongozi hao walikaribishwa kwa baridi na walinzi wanne wa kibinafsi waliokuwa wakilinda migodi hiyo ambapo walinzi hao waliwazuia maafisa kuingia kwenye maeneo ya Madini.

Walinzi wa Nyamutoro na Polisi walifanikiwa kuwapokonya silaha na kuwakamata walinzi hao kabla ya kuwadhuru wakuu wao.

Waziri ameagiza kufungwa mara moja kwa shughuli za uchimbaji Madini hadi taarifa nyingine itakapotolewa.

Share: