Wahamiaji haramu 16 wamekamatwa katika maeneo ya msitu mkoani iringa

WAHAMIAJI haramu wamekamatwa Aprili 06 ,2024 katika maeneo ya Msitu wa Luganga kata ya Sao hill Tarafa ya Ifwagi katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Allan Bukumbi amethibitisha kuwa Wahamiaji hao haramu walitelekezwa katika Mashamba ya Mahindi baada ya kushushwa kwenye gari ambayo awali ilisomeka kwa namba STL 3999 aina ya Landcruiser V8 yenye rangi nyeupe ambayo dereva wake aliitelekeza kwa kufunga milango na kutokomea kusikojulikana.

Kamanda Bukumbi amesema Wahamiaji hao ni raia kutoka nchini Ethiopia ambao bado wanashikiliwa kituoni hapo kwa uchunguzi na Upelelezi zaidi.          

Alisema baada ya uchunguzi wa awali ilibainika kuwa gari hiyo imesajiliwa kwa namba T.803 CVW aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba URJ 202 - 5001217 na injini namba IUR - FE inayomilikiwa na Said Hassan mkazi wa Tabata Dar es salaam. 

Share: