Waendesha mashtaka wa nchi hiyo wanasema kuwa wafungwa hao walitumia mwanya wa uzembe
Idadi kubwa ya wafungwa wametoroka kutoka gereza lenye ulinzi duni nchini Comoro, mamlaka ya nchi hiyo imesema asubuhi ya tarehe 11 Aprili.
Maafisa kutoka visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi walisema wafungwa 38 walitoroka jela hiyo yenye watu wengi katika mji mkuu Moroni, baada ya kusaidiwa na mwanajeshi aliyekuwa kizuizini.
Waendesha mashtaka wa nchi hiyo wanasema kuwa wafungwa hao walitumia mwanya wa uzembe kwenye ulinzi wa gereza hilo kufanikisha azma yao.
Share: