Wafugaji holela kuondolewa namtumbo mkoani ruvuma

Kamati ya Mawaziri Nane wa Kisekta ikiongozwa na Mwenyekiti wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Jerry Silaa imeagiza kuondolewa kwa wafugaji holela katika kijiji cha Likusanguse wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

Silaa ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha Likusanguse wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma walio na makazi yao ndani ya Hifadhi na Mapito ya Wanyamapori ya Selous wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Kisekta wanaosimamia maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi kwa Mkoa wa Ruvuma.

Waziri Silaa amesema Rais Samia aliunda Timu ambayo imefanya maamuzi hayo ya kuondoa wafugaji ambao wanaingiza mifigo yao kwa wakulima na kuanzisha vurugu zinazoleta madhara.

Share: