Wafanyakazi wa shirika la trc watoa siku 30

Baraza Kuu Maalum la Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRAWU) limetoa Siku 30 kwa Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuweka Mkataba wa Hali Bora kwa Wafanyakazi ambao rasimu yake ilikamilika tangu Februari 2023 lasivyo watatangaza mgogoro na Mwajiri wao (TRC)

Mwenyekiti wa TRAWU Taifa, Jacob Shindika, amesema “Kuna daraja ambalo Mtumishi wa TRC anaweza kufanya kazi kwa Miaka 40 akistaafu analipwa Tsh Milioni Moja lakini tunapokuwa na Mkataba wa Hali Bora mambo kama hayo yanajadiliwa na itakuwa msaada kwa Wafanyakazi.”

Share: