Wafanyabiashara, Waongoza watalii na wadau mbalimbali wa Utalii Mkoani Arusha wakijumuika pamoja kuianza safari kuelekea kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro (KIA) kwaajili ya mapokezi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anayeanza ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha leo Novemba 27, 2024.
Wadau hao wa utalii Mkoani Arusha wakiongozwa na Chama cha Mawakala wa Usafirishaji Watalii nchini Tanzania TATO wanaoadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa kwa Chama hicho wanasema wameamua kuungana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kumlaki kwa shangwe Mhe. Rais Samia kutokana na Mchango wake mkubwa na utofauti wake katika utendaji suala lililochagiza ongezeko kubwa la watalii kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Cc; @baba_keagan @ortamisemi @samia_suluhu_hassan @rc_mkoa_arusha @ikulu_mawasiliano
Shiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uwe sehemu ya maamuzi ya mtaa/Kijiji chako kwa maendeleo ya ustawi wa eneo lako.
cc @ortamisemi @mohamed_mchengerwa
#MitaaInaamua
#Novemba27
#NovembaYaMitaa