WAATHIRIKA WA JEFFREY EPSTEIN KUANDAA ORODHA YA WASHIRIKA WAKE

Waathiriwa wa mfanyabiashara Jeffrey Epstein wamesimulia madhila waliyopitia ya unyanyasaji wa kingono wakati wakizungumza mbele ya Bunge la Marekani, huku wakitoa wito kwa wabunge kufichua nyaraka zaidi zinazohusu kashfa ya ngono ya Epstein, aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa hayo.

Lisa Phillips, mmoja wa waathiriwa hao, alisema kundi lao limeanza kuandaa orodha ya siri ya majina ya wahusika waliokuwa karibu na Epstein, wakidai walihusika katika kuwanyanyasa.

“Tunaandaa majina kwa siri, majina ya watu ambao sote tunajua walihusiana mara kwa mara na mtandao wa Epstein,” alisema Phillips. Akasisitiza kuwa kazi hiyo “itafanywa na walionusurika kwa ajili ya walionusurika.”

Hafla hiyo iliandaliwa na baadhi ya wabunge wa Marekani wanaoshinikiza uchunguzi wa Epstein kufunguliwa zaidi na nyaraka zilizofichwa kutolewa hadharani ili ukweli wote ujulikane.

Share: