Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limelaani shambulizi la Jumanne dhidi ya meli ya Norway lililofanywa na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Yemen kutoka Yemen.
Shambulio hilo lilisababisha moto kwenye meli hiyo lakini hakukuwa na majeruhi.
Waasi wa Houthi wameapa kuzuia meli zinazosafiri kwenda Israel hadi pale taifa hilo litakaposimamisha mashambulizi yake mjini Gaza, kwa kile wanachosema ni kuunga mkono Wapalestina.
Kulenga meli za kiraia kwa makusudi au kwa uzembe ni uhalifu wa kivita, HRW ilisema katika taarifa yake siku ya Jumatano.
"Wahouthi wanadai kwamba wanafanya mashambulizi kwa niaba ya Wapalestina, wakati ukweli ni kwamba wanashambulia, kuwaweka kizuizini kiholela, na kuhatarisha maisha ya wasafiri na wafanyakazi wa meli ambao hawana uhusiano wowote na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Palestina ," ilisema.
Mwezi Novemba, wapiganaji wa Kihouthi waliteka meli ya Galaxy Leader ya kubeba magari inayomilikiwa na Uingereza na Japan.