Viongozi wa dini Arusha wamuombea RC Makonda

 Viongozi wa dini mbalimbali wa mkoa wa Arusha wamemfanyia maombi na dua maalumu Mhe. Paul Makonda ambaye ni mkuu wa Mkoa huo baada ya yeye kusimama na kuuombea mkoa huu, watoto, kina mama na kina baba, biashara na uchumi wa mkoa huu uweze kuimarika.