Vifo vya uzazi vimepungua kwa asilimia 80 'Rais Samia Suluhu Hassan'

Mapema Jijini Dar es Salaam, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nimepokea Tuzo ya The GoalKeepers Award inayotolewa na Taasisi ya Gates Foundation.

Tuzo hii ni heshima kubwa kwetu Watanzania kwani mbali na sisi kufurahia matunda ya hatua kubwa tunazoendelea kupiga katika sekta ya afya, inadhihirisha dunia inatambua juhudi zetu katika kuboresha afya ya uzazi na afya ya Mama na Mtoto.

Nchi yetu imefanya kazi kubwa na ya kujivunia, ambapo mpaka sasa tumefanikiwa kupunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 80%, kutoka vifo 556 kwa kila vizazi 100,000 hadi 104; na vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 67 hadi 43 kwa kila vizazi 1,000.

Kazi hii njema inaendelea ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu wa afya, kutoa huduma za afya bure kwa akina mama na watoto, kuanzisha programu za lishe, kuimarisha mifumo ya rufaa, kuboresha huduma za dharura na kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya afya mijini na vijijini.

Tuzo hii naielekeza kwa watumishi wa afya kote nchini kwa kazi kubwa wanayofanya usiku na mchana kuwahudumia Watanzania, lakini pia kwa washirika wetu na wadau wa maendeleo katika kazi ya kuboresha afya ya 

Share: