Upepo ulioambatana na mvua wasababisha madhara momba mbunge atoa pole

Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe (Mundy) amefika na kutoa pole kwa wakazi wa Vijiji Vya Ntinga na Msangano kufuatia baadhi yao kukubwa na kadhia ya Nyumba zao kubomoka kwa Mvua iliyoambatana na upepo mkali.

Akiwa eneo la tukio Mhe. Condester pia amechangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kurudishia paa kwenye darasa la shule ya Msingi Msangano ambalo pia liliezuliwa na upepo huo.

"Nawapa pole sana Waathirika wa upepo huo, tuendelee kuchukua thahadhari kwani taarifa za mamlaka ya hali ya hewa zinaonyesha kuwa musimu huu Mvua zinaweza kuwa nyingi"Sichalwe.

Share: