Kauli hiyo imetolewa na Profesa Barnabas Nawangwe, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho
Chuo Kikuu cha Makerere kimesema takriban Wanafunzi 1,000 wanaacha au kuachishwa Masomo kila Mwaka chuoni hapo kutokana na kupoteza Fedha za Ada wanazozitumia kwenye Michezo ya Kubashiri maarufu kama 'Kubeti'
Kauli hiyo imetolewa na Profesa Barnabas Nawangwe, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho ambaye amesema Chuo kililazimika kufanya tafiti kujua sababu za Wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo
Aidha, kwa mujibu wa takwimu za Drive Research, Sekta ya Michezo ya Kubashiri (Betting) Duniani kote ilikadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Dola Bilioni 235 (zaidi ya Tsh. Trilioni 599.25) kwa Mwaka 2022 huku ikiwa na Wacheza Kamari takriban Milioni 176, idadi hiyo inatajwa itafika Watu Milioni 210 Mwaka 2025