Jehi la Polisi Mkoani Tanga limeitaka Jamii kushirikiana na Jeshi hilo Kutokomeza ukatili wa Kijinsia na watoto kwa kutoa Taarifa ya matukio hayo ili kudhibiti matukio ya Ulawiti, ubakaji unaofanywa na baadhi ya Waalimu, ndugu na bodaboda ambao sio waaminifu kwenye jamii
Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Handeni Enock Chimaguli kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi wakati wa kupokea Vitendea kazi kutoka Taasisi ya @hope4young_girls zitakazosaidia upatikanaji na Utunzaji wa Taarifa za Ukatili wa Kijinsia na watoto pamoja ba Uzinduzi wa Dawati la Jinsia kituo cha Polisi Mkata, Wilayani Handeni mkoani Tanga
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hope 4 Young Girls @salama_kikudo ameitaka Jamii kuungana kwa pamoja ili kuweka nguvu katika maeneo wanayoishi ili kuweza kutokomeza ukatili wa Kijinsia ambao umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo, Uchumi pamoja na kukandamiza haki za watoto, wasichana na wanawake katika kila nyumba