Tunafanyia kazi malalamiko

katika mikutano itumike lugha nzuri na maneno yenye staha yasiyoudhi wengine ili kutovunja misingi ya Amani

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda amewashauri wananchi kutodharau maoni yanayotolewa na vyama vya upinzani kwakua baadhi ya mambo wanayoyasema yanaisaidia serikali kufanyia kazi na wananchi kunufaika na huduma mbalimbali za kijamii

Makonda ameyasema hayo eneo la Kisesa Jijini Mwanza wakati akiwasikiliza wananchi wa eneo hilo ambapo amebainisha faida wanazopata kutoka kwenye baadhi ya malalamiko ya vyama vya upinzani ni kujua pale paliposahaulika naku pashughulikiwa kwa haraka na ndio maana Rais wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vyote bila ubaguzi.

Amesema Tanzania ni nchi inayotekeleza misingi ya kidemocrasi duniani ila onyo katika mikutano hiyo itumike lugha nzuri na maneno yenye staha yasiyoudhi wengine ili kutovunja misingi ya Amani,Umoja na Mshikamano uliopo nchini.
Share: