Trafiki aliyegongwa na gari  aagwa leo

Mwili wa askari wa kitengo cha usalama barabarani Sajenti Stella Alphonce, aliyefariki dunia jana baada ya kugongwa na gari la shule, umeagwa katika kanisa katoliki kigango cha Isegenge, Kata ya Nyakato jijini Mwanza kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa mazishi.

Miongoni mwa walioshiriki maombolezo hayo ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza ACP Wilbroad Mutafungwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi. 

Askari huyo alifariki jana Jumatano katika eneo la Nyamuhongolo Jijini Mwanza, baada ya kugongwa na gari la shule wakati akiendelea kutekeleza majukumu yake.

Share: