Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zetech Nchini Kenya amefariki kwa Kujinyonga huku akiacha barua aliyoiandika kwenye ukurasa wake Facebook akidai kuwa sababu iliyompelekea kuchukua uamuzi huo ni ugumu anaowekewa na Ma Lecturer wa Chuo hicho na kukosa hudumu kutoka kwa Mama yake ambae ni Single Mother.
Ujumbe mrefu uliochapishwa kwenye akaunti yake ya Facebook siku moja iliyopita, mnamo Jumanne, Desemba 10, amedai kuwa Lecturer mmoja wa Kike amekuwa akimpunguzia Alama zake ili kumfelisha kwenye masomo yake.
“Fikiria unapambana na ndoto zako alafu mtu anajaribu kuuwa matumaini madogo uliyojiwekea”
Mbali Na hivyo amemlaumu Mama yake kwa kushindwa kumuhudumia kwa kutokumlipia kodi Mpaka kuamua kuishi maisha ya uongo chuoni.
Pia aliongeza kuwa kusema kuwa kulelewa na Single Mother inafanya mtoto WA kiume apitie magumu sana.
Mwili wa mwanafunzi huyo uligunduliwa ukining'inia kwenye paa la jengo saa chache baada ya chapisho lake la Facebook.