Tarura yawaunganisha wananchi wilaya ya ruangwa na liwale

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Lindi imekamilisha ujenzi wa daraja la Mbwemkuru lenye urefu wa mita 75 na kufungua barabara ya Ruangwa-Nangurugai- Kiangara-Mirui-Mbwemkuru yenye jumla ya Km 65.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Ruangwa, Mhandisi Mashaka Narubi ameeleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo imekua ni fursa kwa wananchi kusafiri kwa urahisi kutoka Ruangwa kwenda Liwale.

"Daraja hili ni muhimu kwa wananchi wa wilaya zote mbili katika kusafiri na kusafirisha bidhaa na mazao, tumejenga daraja na kufungua barabara na sasa magari yanapita hapa kwenda Liwale ", amesema mhandisi Narubi.

Bi. Sharifa Majaliwa mkazi wa Kijiji cha Nangurugai amesema kuwa kabla ya kujengwa Daraja hilo ilikuwa vigumu kwao kufanya shughuli za kilimo ng'ambo ya pili ya mto lakini kwa sasa wanavuka na kufanya kazi zao kwa urahisi.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mirui, Bw. Chande Ally amesema kuwa mwanzoni Kijiji hicho kilikuwa hakifikiki kwani mtu alikuwa hawezi kutoka Mirui kwenda Ruangwa kwa urahisi.

Share: