Tanzania, austria kushirikiana elimu ya ufundi, utalii, biashara na uwekezaji

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Austria zimekubaliana kuimarisha sekta za elimu ya ufundi pamoja na utalii.

Makubaliano hayo yameafikiwa katika Mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angelah Kairuki (Mb) na Waziri wa Kazi na Uchumi wa Austria, Mhe. Prof. Martin Kocher walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam.

Waziri Kairuki amesema kuwa wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya kilimo, elimu ya ufundi ambapo Tanzania kwa sasa msukumo wake ni elimu ya ufundi na tayari serikali imeanza kuboresha sera ya elimu na mitaala ya elimu.

Share: