Aidha baada ya mshtakiwa kusomewa kosa na maelezo ya kosa, Wakili wa Jamhuri ambaye ni Mwanasheria wa TAKUKURU Bw. Emmanuel Chipanta, aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo usiku wa Januari 5, 2024, ambapo mshtakiwa alikiri kosa na kutiwa hatiani.
Januari 8, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Muheza, katika Shauri la Jinai CC. 544/2024, yametolewa maamuzi ambapo mshtakiwa Bw. Adam David Mbasha, Mhandisi wa Umeme, mwajiriwa wa Kampuni ya Red Farm, inayotekeleza kandarasi ya kusambaza umeme vijijini, ametiwa hatiani na kuhukumiwa kulipa faini ya Tshs. 500,000/- kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2022.
Shitaka hilo limefunguliwa Januari 8, 2024, ambapo Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani kwa shtaka la kuomba na kupokea Rushwa kiasi cha TSh. 30,000.00 kutoka kwa Costas Thomas Mabondo, mkazi wa Muheza, ili aweze kumwekukea mita ya umeme kwenye nyumba yake bila kufuata utaratibu.