Takriban watu 12 wamefariki na zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi nchini kongo

Takriban watu 12 wamefariki na zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kusababisha bonde kuporomoka kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.kwa mujibu wa afisa wa eneo hilo

Maporomoko ya ardhi yalitokea Jumamosi saa sita mchana katika wilaya ya Dibaya Lubwe katika jimbo la Kwilu.

Mafuriko hayo yalisomba na kupeleka udongo na uchafu kwenye ukingo wa Mto Kasai, ambapo mashua ilikuwa ikitia nanga na watu walikuwa wakifua nguo.

Gavana wa muda wa mkoa Felicien Kiway alisema miili 12 imetolewa kwenye vifusi hadi sasa, ikiwa ni pamoja na wanawake tisa, wanaume watatu na mtoto mchanga.

"Takriban watu 50 hawajulikani walipo lakini tunaendelea kupekua udongo," alisema na kuongeza kuwa uwezekano wa kupata manusura ulikuwa mdogo kwani tukio hilo lilitokea saa 12 kabla.

Mratibu wa jumuiya ya kiraia ya eneo hilo, Arsene Kasiama, alisema maporomoko hayo pia yaliangukia watu waliokuwa wakinunua bidhaa sokoni.

Alitoa idadi ya vifo vya watu 11, na manusura saba waliojeruhiwa vibaya na zaidi ya watu 60 wakiwa hawajulikani waliko Mipango duni ya mijini na miundombinu duni kote Kongo hufanya jamii kuwa katika hatari zaidi ya mvua kubwa, ambayo inazidi kuongezeka mara kwa mara barani Afrika kulingana na wataalam wa hali ya hewa.

Share: