Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe Japhari Kubecha amezitaka shule zote za Serikali ambazo ni Msingi na Sekondari kuhakikisha waanzisha Klabu ya Zimamoto na Uokoaji zitakazowasaidia kuwajenga wanafunzi umuhimu wa kudhibiti majanga ya moto na namna ya kujitolea
Japhari Kubecha ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Wazimamoto wa Kujitolea na Klabu za Zimamoto wilaya ya Tanga ambapo amesema kumekuwa na tabia ya watu kurekodi video za ajali Barabarani badala ya kusaidia watu waliopata majanga ambapo kupitia Klabu hizo watakuwa Wazalendo pindi majanga yanapotokea.
Aidha ameagiza vijana hao kupewa vyeti vya Klabu ya Zimamoto watakapohitimu masomo yao katika shule ili waweze kutambulika ambao pia watakuwa na msaada kwa jamii pindi wajanga ya moto yatakapotokea.
Pia amezitaka Kata zote Jijini Tanga kutoa uwakilishi wa Vijana wasiopungua watano ambao wataenda kuingia kwenye Mpango Mkakati wa Klabu ya Mafunzo ya Wazimamoto wa Kujitolea