Sgr: wafanyakazi wagoma wakidai kutolipwa mishahara yao toka desemba 2023

Baadhi ya Wafanyakazi wanaoshiriki katika Ujenzi wa Mradi wa Reli ya SGR wameshiriki katika mgomo wa kutofanya kazi leo Jumamosi Januari 6, 2024 kutokana na kinachodaiwa kutolipwa mishahara yao ya Desemba 2023.

Licha ya kupunguza wafanyakazi zaidi ya 600 hivi karibuni Mkandarasi Mkuu wa SGR, Yapi Merkezi hajakamilisha malipo hayo ya Desemba huku kukiwa hakuna taarifa rasmi juu ya kinachoendelea au lini malipo yatafanyika.

Taarifa zilizopatikana ni kuwa Wafanyakazi waliogoma ni wa Ilala, Dar es Salaam, Tabora, Dodoma pamoja na wale wa Kambi ya Itigi Mkoani Singida, ambapo wanataka uongozi wa Yapi utoe majibu juu ya malipo ya stahiki zao hizo

Share: