Serikali yatoa tamko kuhusu taarifa za virusi vya Marburg Kagera

Wizara ya Afya imepokea tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera.

Kufuatia tetesi hizo, Wizara imechukua hatua kadhaa za haraka ikiwemo: kutuma timu ya wataalamu; kufanya uchunguzi wa suala hili; kuchukua sampuli na kufanya vipimo vya maabara. Mpaka leo, tarehe 15 Januari 2025, majibu ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa wahisiwa wote waliochukuliwa sampuli hizo hayajathibisha uwepo wa virusi vya Marburg.

Wizara inapenda kuwahakikishia wananchi pamoja na jumuiya ya kimataifa, likiwemo Shirika la Afya Duniani (World Health Organisation - WHO), kuwa imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na itaendelea kutoa taarifa zaidi.


Share: