Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohammed Hassan Moyo amasema kuwa maazimisho hayo ni jitihada za serikali katika kuendelea kutoa Elimu kuhusu masuala ya lishe na afya kwa ujumla. Pia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora kutoka katika makundi sita (6) huleta matokeo mema ya Afya bora.
Sambamba na hilo Mhe. Moyo amesema kwasasa magonjwa yasiyoambukiza yameongezeka kwa asilimia 5% ukilinganisha na miaka ya 1980's na magonjwa hayo ni kisukari, moyo, figo, saratani, shinikizo la damu na nakadhalika, na ili kuepuka magonjwa haya yatupasa kula vyakula vyenye lishe bora na kushughulisha mwili kwa mazoezi.
Pia mpango huu wa elimu ya lishe ni dhumuni la serikali katika kuwahudumia wananchi kuhusu masuala ya Afya katika makundi maalum ya watoto na mama wajawazito, vijana, wazee, aidha katika Taasisi mbalimbali ikiwemo Mashuleni ili kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu ya kutosha kuhusu Lishe na Afya kwa ulaji bora na mazoezi.
Aidha akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Mganga mkuu wa wilaya ya Nachingwea Ndugu Ramadhani Mahige ameeleza umuhimu wa siku hiyo na kuwaambia wananchi watapata fursa ya kupima bure magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, kisukari, uzito, urefu nakadhalika ili kutambua hali zao kiafya.
Pia wananchi wameshukru maazimisho hayo ya lishe kitaifa na wameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali katika sekta ya Afya kwa ujumla