Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inathamini na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari katika kufanikisha kazi yao muhimu ya kuhabarisha umma juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa ya kukamatwa kwa Mwandishi Dickson Ng’hily na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo iliyoleta taharuki kwa wananchi na waandishi wa habari huku ikidai mwandishi huyo hakupigwa wala kuvunjiwa simu yake.
Taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini imebainisha Ukweli ni kwamba mwandishi huyo hakupingwa na mtu yeyote isipokuwa aliulizwa na Mwalimu Mkuu kwa nini anapiga picha bila ridhaa yao wala kujitambulisha.
“Baada ya mwandishi huyo kukataa kutoa ushirikiano alipelekwa ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye akapelekwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwaajili ya kujiridhisha kama kweli ni mwandishi na ana kibali cha kufanya kazi hiyo.” imeeleza taarifa hiyo.
“Aidha, ni kweli kuwa wanafundi walikuwa nje ya madarasa yao kwaajili ya progeamu maalum ya kufanya masahihisho ya mitihani wa Utamilifu (mock) Mkoa, hivyo kimsingi shule haina wanafunzi wanaosomea nje kwa kukosa madarasa.”
“Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inathamini na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari katika kufanikisha kazi yao muhimu ya kuhabarisha umma juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo. Hata hivyo, ni muhimu waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo katika kutimiza haki yao ya kutafuta, kuchakata na kusambaza habari.”