Daraja la J.P. Magufuli (pia likijulikana kama Kigongo–Busisi Bridge) lilizinduliwa rasmi tarehe 19 Juni 2025 huko Mwanza na Rais Samia Suluhu Hassan, tukio lililotangazwa na Waziri Ujenzi Abdallah Ulega na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,huku shamra shamra za wananchi na wadau mbali mbali zikisheheni .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa km 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 katika eneo la Kigongo, Misungwi mkoani Mwanza tarehe 19 Juni, 2025. Daraja hilo ambalo ni sehemu ya barabara ya Usagara-Sengerema-Geita ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Sirari hadi Mtukula na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi Februari, 2020.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa km 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 katika eneo la Kigongo, Misungwi mkoani Mwanza tarehe 19 Juni, 2025. Daraja hilo ambalo ni sehemu ya barabara ya Usagara-Sengerema-Geita ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Sirari hadi Mtukula na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi Februari, 2020.