Same: mhasibu wa halmashauri ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka

Fedha hizo ni makusanyo ya kila Siku kutoka kwa Wagonjwa ambazo hakuzipelekwa Benki

Mahakama ya Wilaya ya Same imemhukumu Paulo Ngiloriti Teveli aliyekuwa Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Same, kifungo cha Miaka 20 jela kwa Makosa ya Matumizi mabaya ya Madaraka na ubadhirifu wa Tsh. 8,377,000. 

Fedha hizo ni makusanyo ya kila Siku kutoka kwa Wagonjwa ambazo hakuzipelekwa Benki kwa kipindi cha Mwaka 2020. 

Aidha, pamoja na adhabu hiyo Mshtakiwa ametakiwa kurejesha fedha zote (Tsh. 8,377,000) ambazo ni mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Same. 

Share: