Rushwa ndogo ndogo zinawakera wananchi - simbachawene

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema kuna haja ya kutengeneza sheria za kuwashughulikia viongozi walioshiriki katika masuala ya rushwa wanapostaafu ili kutoa funzo kwa viongozi wengine.

Simbachawene, amesema hayo Leo Novemba 20,2023 jijini Dodoma , wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Amesema rushwa ndogondogo bado zipo na zinawakera wananchi hivyo lazima kuwa na mikakati ya kuhakikisha zinazuiliwa.

Ameongeza kuwa :”Mtu anapostaafu kama alishiriki katika uozo lazima ashughulikiwe tukifanya hivyo tutakuwa tunatoa somo kwa viongozi wengine.Tusipo shughulikiana tutakuwa hatusemi ukweli kwa Taifa letu kwasababu rushwa bado ni tatizo.

Simbachawene amesema bado yapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwepo kwa rushwa katika taasisi mbalimbali hali ambayo inasababisha wananchi kukosa huduma ambazo wanazihitaji.

Na kuongeza kuwa :”Huduma hizo ni pamoja na elimu ngazi za chini kati hadi vyuo vikuu, lakini pia huduma za afya,kodi na leseni ambako kumewekwa utaratibu mgumu wa upatikaji wa huduma ili tuu watu watoe rushwa.

Share: