RC Makonda, Viongozi wa dini kuongoza maombi maalumu kwa mkoa wa Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda anakualika wewe mwananchi wa Mkoa wa Arusha tarehe 09 Disemba 2024, kushiriki pamoja kwenye Siku maalum ya kuuombea Mkoa wa Arusha dhidi ya changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa huu pamoja na watu wake kwa ujumla.

Ratiba ya siku hiyo maalum kwaajili ya kujifungamanisha na Mwenyenzi Mungu itafanyika kuanzia saa Mbili kamili asubuhi, ambapo Mhe. Makonda amesema shughuli hiyo itaanza na matembezi ya pamoja yatakayoongozwa na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini yakianzia kwenye mzunguko wa barabara ya Impala (Impala Round about)na hitimisho lake likiwa kwenye Mzunguko wa barabara ya mnara wa Uhuru Jijini Arusha.

"Tarehe Tisa Disemba mwaka huu tutatembea tukiwa na bendera zetu tukiombea juu ya Ardhi ya mkoa wetu wa Arusha. hatutaki mtu aanze biashara yake Mkoani Arusha afilisike, hatutaki mtu asomeshe mtoto wake Arusha afeli, hatutaki mtu Azae mtoto wake Arusha halafu afe katika umri mdogo. Tunataka kila kitakachoanzishwa Arusha tukitabiria na kukitangaza tarehe Tisa siku ya uhuru ya kwamba tupo huru kwaajili ya mafanikio yetu." Amesema Mhe. Makonda.


Share: