Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumapili Novemba 17, 2024 ameongoza maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Arusha kwenye kuwaombea Kheri manusura wa ajali ya kuporomoka kwa Jengo la Ghorofa nne katika makutano ya Mtaa wa Congo na Mchikichi, Kariakoo Jijini Dar Es salaam.
Kulingana na Mrakibu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Dar Es salaam Bw. Peter Mtui amewaambia wanahabari kuwa watu watano wamefariki dunia katika ajali hiyo, huku wengine 45 wakijeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi ya Jumamosi ya Novemba 16, 2024 na mpaka hivi sasa jitihada mbalimbali za uokozi zinaendelea.
Share: