Miaka minne baada ya kuzuiwa na Serikali ya Marekani kuingia nchini humo yeye na Mkewe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumapili Novemba 17, 2024 amesema hatishwi na maamuzi hayo na msimamo wake wa kupingana na vitendo vya Mapenzi ya jinsia moja na usagaji bado upo pale pale na hautabadilika
RC Makonda wakati huo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Ijumaa ya Januari 31, 2020 ilimpiga marufuku kuingia nchini Marekani akituhumiwa kushiriki katika ukandamiza wa haki za binadamu na kuwa kikwazo kwa watu kujiamulia mambo yao.
Leo Jumapili akizungumza na Wanahabari na wananchi wa Arusha kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano Jijini Arusha AICC wakati akitoa tathimini ya Utendaji wake kwa miezi sita ya awali, Mhe. Makonda amesema kamwe hatokubali maamuzi ya kufanya vitendo hivyo vya Mapenzi ya jinsia moja kuwa sehemu ya haki za binadamu, akiwataka pia viongozi wengine kote duniani kukemea mambo hayo kwani hayampendezi Mwenyenzi Mungu na si salama kwa vizazi vijavyo.