Rc chalamila serikali itaendelea kuboresha mazingiara ya wafanyabiashara dsm

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo katika mkutano wa Shirikisho la wenye viwanda (CTI) katika Ukumbi wa Hotel ya Four Point posta Ilala Jijini Dar es Salaam

RC Chalamila amesema Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekua mstari wa mbele katika kuboresha mazingira ya wafanyabishara wakati wote amekua msikivu kusikiliza kero zao na kuzitatua ndio maana katika ziara zake nje ya nchi amekua akiambatana na wafanyabishara, wamiliki wa viwanda ili kutanua fursa za kibiashara ndani na nje. " Ni ukweli usiopingika unapoongelea suala la "Private and Public pertnership" Rais Dkt Samia ndio Champion namba moja " Alisema RC Chalamila

Aidha Mhe Chalamila ametoa nafasi kwa wafanyabishara kueleza kero na Changamoto mbalimbali, maoni na ushauri kwa lengo la kuboresha sekta hiyo, ambapo alitolea majibu Changamoto zilizoko ndani ya uwezo wake na zile ambazo ziko nje ya uwezo ameahidi kupeleka mamlaka husika.

Sambamba na hilo RC Chalamila amesema lazima tuendelee kumshukuru Mhe Rais Dkt Samia na kuunga mkono juhudi zake katika sekta ya biashara hapa nchini amekua akiwekeza kwa kiasi kikubwa katika miundombinu ya barabara, reli, Anga katika historia ya nchi hii hatukuwai kuwa na ndege kubwa ya mizigo lakini saizi ipo, hiyo haitoshi anaendelea kuweka sera nzuri ya uwekezaji na kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ili ikidhi vigezo vya Kimataifa kwa masilahi mapana ya watu wengi

Share: